https://utafitionline.com/index.php/jkal/issue/feed Journal of Kiswahili and Other African Languages 2025-01-13T09:31:18+00:00 Open Journal Systems <p>The <strong>Journal of Kiswahili and Other African Languages</strong> is a high quality open-access, peer-reviewed and refereed multidisciplinary research journal, dedicated to serve the society by the global dissemination of information through an unparalleled commitment to quality, reliability, and innovation and research work. Journal of Kiswahili and Other African Languages welcomes and acknowledges high quality theoretical and empirical original research papers, case studies, review papers, literature reviews and conceptual framework from researchers, academicians, professional, practitioners and students from all over the world. Journal of Kiswahili and Other African Languages engages its noble efforts for the development and endeavours to give you the best.</p> https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/884 Uhifadhi wa Utamaduni kupitia Mchakato wa Tafsiri: Mifano ya Tafsiri ya Riwaya za Kaburi Bila Msalaba na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka, Ntulanalwo na Bulhawali 2025-01-13T09:31:18+00:00 Nyatichi Makini Georginahmakini1@gmail.com Nathan Ogechi Georginahmakini1@gmail.com Mosol Kandagor Georginahmakini1@gmail.com <p>Tafsiri ni mchakato wa kuhawilisha mawazo au ujumbe ulio katika lugha ya maandishi kutoka lugha chanzi kwenda katika lugha lengwa. Taaluma ya tafsiri inatumika kama nyenzo ya kueneza utamaduni, maarifa mapya, ujuzi, na uzoefu kutoka kwa jamii moja kwenda nyingine. Makala hii inakusudia kueleza jinsi utamaduni wa Kiafrika unadumishwa na kuhifadhiwa kupitia mchakato wa tafsiri. Makala iljikita katika uchanganuzi wa tafsiri ya <em>Kaburi Bila Msalaba </em>(1969) na<em> Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali</em> (1981). Makala hii ilipania kutoa maelezo jinsi tafsiri ya riwaya hizi ambazo ni hazina ya hifadhi ya utamaduni wa Kiafrika, inavyochangia na kuendeleza uhifadhi wa utamaduni kutoka lugha moja hadi nyingine. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya <em>Skopos </em>inayosisistiza lengo la tafsiri kuzingatiwa kabla ya zoezi la tafsiri kuanza. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kusoma na kuchambua matini chanzi <em>Kaburi Bila Msalaba </em>na<em> Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali </em>na matini lengwa, <em>Unmarked Grave </em>na<em> Mr. Myombekere and His Wife Bugonoka, Their son Ntulanalwo and Daughter Bulihwali</em>. Makala hii ililenga kuangazia vipengele vya kitamaduni vilivyohawilishwa kutoka utamaduni chanzi na kuingizwa kwa utamaduni lengwa na jinsi vinavyochangia uhifadhi wa utamaduni katika jamii mahususi. Mkabala wa kitaamuli ulitumika katika uwasilishaji wa data. Matokeo yalidhihirisha kwamba vipengele vya kitamaduni vimehawilishwa kutoka lugha moja kwenda nyingine hivyo basi, uhifadhi wa utamaduni umewezeshwa kupitia mchakato wa tafsiri.</p> 2025-01-15T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2025