Journal of Kiswahili and Other African Languages https://utafitionline.com/index.php/jkal
The Journal of Kiswahili and Other African Languages is a high quality open-access, peer-reviewed and refereed multidisciplinary research journal, dedicated to serve the society by the global dissemination of information through an unparalleled commitment to quality, reliability, and innovation and research work. Journal of Kiswahili and Other African Languages welcomes and acknowledges high quality theoretical and empirical original research papers, case studies, review papers, literature reviews and conceptual framework from researchers, academicians, professional, practitioners and students from all over the world. Journal of Kiswahili and Other African Languages engages its noble efforts for the development and endeavours to give you the best.
en-US

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
Tue, 24 Jun 2025 12:02:02 +0000 OJS 3.3.0.16 http://blogs.law.harvard.edu/tech/rss 60 Mikakati ya Utetezi wa Mazingira katika Riwaya za Nakuruto na Bustani Ya Edeni https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1105
Makala haya yanalenga kutathmini utetezi wa mazingira katika riwaya za Nakuruto (2009) ya Clara Momanyi na Bustani ya Edeni (2001) ya Emmanuel Mbogo. Kufuatia uharibifu wa mazingira kote ulimwenguni, utetezi wa mazingira umekuwa ukifanyika katika majukwaa mbalimbali yakiwemo makongamano ya kimataifa, mashirika ya uanaharakati na katika vyombo vya habari. Katika miaka ya hivi karibuni wanafasihi pia wameanza kutumia fasihi kama jukwaa la utetezi wa mazingira katika kazi zao za riwaya, tamthilia, hadithi fupi na ushairi. Jambo hili ndilo lililomvutia mtafiti kuchunguza namna suala la utetezi wa mazingira lilivyoshughulikiwa katika riwaya teule. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki-Ikolojia kwa mujibu Glotfelty (1996). Muundo wa utafiti huu ni wa kimaelezo. Sampuli ya utafiti huu ni riwaya za Nakuruto (2009) na Bustani ya Edeni (2001) ambazo ziliteuliwa kimakusudi ili zichunguzwe. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa mikakati mbalimbali kama vile dini, sheria, vyombo vya habari, mabango, nyimbo na maandamano imetumika kuyatetea mazingira. Makala haya yatawachochea wanaharakati wa mazingira katika kutumia majukwaa mbalimbali kuyatetea mazingira. Aidha, utafiti huu utapiga jeki juhudi za Wizara ya Mazingira katika kuhamasisha jamii kuhusu uharibifu dhidi ya mazingira.
Erick Maina, Lina Akaka, Rose Mavisi Copyright (c) 2025 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1105 Tue, 24 Jun 2025 00:00:00 +0000 Usawiri wa Ujumi katika Fasihi Simulizi: Uchambuzi wa Ngano za Wahehe https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1130
Lengo la makala hii ni kujadili namna ujumi unavyosawiriwa katika fasihi simulizi, hususani ngano za Wahehe. Kusawiriwa kwa ujumi katika ngano za Wahehe kupitia vipengele vya ujumi kumeweka bayana uwiano wa vipengele hivyo na jamii husika. Aidha, athari zake kwa jamii husika zimebainishwa. Utafiti uliozaa makala hii ulitumia mbinu za kitaamuli. Data zilikusanywa kwa kutumia njia za uchambuzi matini na mahojiano. Ngano teule zilipatikana kwa kutumia sampuli lengwa. Utafiti na mjadala vimefanywa kwa kutumia Nadharia ya Ki-Marx iliyoasisiwa na Karl Marx na Fredrick Engels. Nadharia hii imekuwa faafu katika utafiti wa makala hii kwasababu inatumia mbinu za kipembuzi katika kuchanganua masuala ya kijamii na kiutamaduni. Matokeo yameonesha kwamba ujumi unaweza kusawirika katika ngano za Wahehe kupitia vipengele vyake, ambavyo ni ujumi katika mtu, asili, vitu, na sanaa. Aidha, vipengele hivyo vinaweka wazi idili za jamii husika zinazotokana na masuala mbalimbali yaliyopo kwenye jamii kama vile uongozi, malezi, ndoa, ufugaji, ulinzi, na kilimo.
Neema Julius Luhwago Copyright (c) 2025 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1130 Sat, 12 Jul 2025 00:00:00 +0000 Uchanganuzi wa Mofu katika Kauli Mbalimbali za Mnyambuliko wa Vitenzi vya Silabi moja: Lahaja ya Ginantuzu https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1151
Suala la mfuatano wa mofu katika kauli za vitenzi limewavuta wanaisimu wengi. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanyika katika Kisukuma lahaja ya Ginantuzu kuhusu mfuatano wa mofu katika kauli za vitenzi vya silabi moja. Kwa hiyo, makala hii ililenga kuchunguza uchanganuzi wa mofu katika kauli mbalimbali za mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja katika lahaja ya Ginantuzu. Lengo la makala hii lilikuwa kuchunguza vitenzi vyenye silabi moja na kubainisha mfuatano wa mofu katika kauli za vitenzi katika lahaja ya Ginantuzu. Utafiti ulifanyika katika kata za Sapiwi na Matongo wilaya ya Bariadi Vijijini. Vijiji viwili vilipitiwa na mtafiti. Vijiji hivyo ni Igegu na Matongo. Jumla wa watoataarifa 20 walifikiwa kwa uwiano sawa wa kijinsia. Vitenzi 80 viliteuliwa na mtafiti na kuwekwa katika kategoria mbili; vitenzi visoukomo katika kundi moja na vitenzi vya silabi moja katika kundi jingine na kupelekwa kwa watoataarifa. Watoataarifa waliteuliwa kwa kuzigatia kigezo cha usampulishaji lengwa. Data za makala zilikusanywa kwa mbinu ya Ushuhudiaji, mahojiano, hojaji na mapitio ya nyaraka za maktabani, makavazi na mitandaoni. Kama mwongozo wa kazi hii, makala imetumia nadharia ya Kanuni Tazamishi (KAT). Aidha, Mkabala wa kitaamuli ndio umetumiwa kubainisha mfuatano wa mofu na kauli. Matokeo ya makala ilibaini kauli sita (6) za vitenzi. Jumla ya vitenzi kumi vya silabi moja katika lahaja ya Ginantuzu vilipatikana. Makala pia imeonesha kuwa, baadhi ya vitenzi vya silabi moja havikubali kupokea baadhi ya mofu za kauli husika. Kikanuni, upangaji wa kauli hizi sio wa kubandika tu bali unafuata kanuni ya utokeaji wake.
Njana Masanja Copyright (c) 2025 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1151 Tue, 15 Jul 2025 00:00:00 +0000 Mofosemantiki na dhima ya Majina ya Ng’ombe kwa Kigezo cha Rangi: Mifano kutoka Jamiilugha ya Ginantuzu https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1155
Makala hii inahusu uchunguzi wa mofolojia na semantiki katika majina ya ng’ombe kwa kigezo cha rangi hususani katika jamiilugha ya Ginantuzu. Lengo kuu la makala hii ni kubainisha maumbo yaliyomo katika majina ya ng’ombe, maana na dhima za majina ya ng’ombe. Utafiti huu ulifanywa katika mkoa wa Simiyu, wilaya ya Bariadi vijijini. Jumla ya vijiji viwili vilipitiwa na mtafiti. Vijiji hivyo ni Ihusi na Nkindwabiye. Sampuli ya watoataarifa sita (6) iliteuliwa na mtafiti kwa ajili ya mahojiano ili kukidhi lengo la makala hii. Kwa kutumia usampulishaji lengwa wastani wa watoataarifa (3) kwa kila kijiji walipatikana. Watoataarifa waliteuliwa kwa kuzigatia kigezo cha usampulishaji lengwa. Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano, ushuhudiaji na mapitio ya nyaraka za maktabani na mitandaoni. Ili kufanikisha kazi hii, makala ilitumia nadharia ya Semeotiki iliyoasisiwa na Ferdinand de Saussure. Aidha, Mkabala wa kitaamuli ndio umetumiwa kubainisha maumbo, maana na dhima za majina ya ng’ombe. Matokeo yameonesha kuwa majina ya ng’ombe dume yameundwa kwa mashina ya ng’ombe jike kwa kuongezewa mofu tangulizi inayobeba maana ya dume. Jumla ya alomofu tatu zinazobanisha jinsia ya kiume zilipatikana. Alomofu hizo ni gί-, gid- na gida-. Mwisho makala hii inapendekeza uchunguzi zaidi wa kiisimu kuhusu utoaji wa majina ya mifugo kuendelea kufanyika ili kuimarisha mawasiliano katika jamii mbalimbali za wafugaji na kuyahifadhi majina hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Njana Masanja Copyright (c) 2025 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1155 Wed, 16 Jul 2025 00:00:00 +0000 Tamathali za Usemi na Uchimuzi wa Maudhui ya Mamlaka katika Asali Chungu https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1328
Lengo la makala haya ni kuchunguza jinsi Said Ahmed Mohamed anavyotumia tamathali za usemi mbalimbali kama vipengele vya kimtindo katika kuibua maudhui ya mamlaka katika riwaya yake ya Asali Chungu. Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Uchimuzi, hasa mhimili wa ukiushi wa nadharia hiyo. Data ilikusanywa kwa kunakili madondoo kutoka katika riwaya ya Asali Chungu. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kulenga madondoo yanayochimuza maudhui ya mamlaka katika riwaya hiyo. Uchanganuzi wa data ulifanywa kitaamuli kwa kutambulisha ruwaza na mienendo ya kiisimu iliyobainika katika madondoo. Kisha, uamilifu wa ruwaza na mienendo hiyo ulichanganuliwa kwa kuzingatia muktadha wa ruwaza na mienendo hiyo, mintarafu suala la mamlaka. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba sitiari na kinaya ndizo tamathali za usemi zilizotumiwa hasa na mwandishi kusawiri maudhui ya mamlaka katika riwaya yake. Utafiti huu unapendekeza kwamba uchunguzi kuhusu tamathali za usemi uhusishwe na vipengele vingine vya kimtindo kama vile kipengele cha kileksika na cha kisintaksia.
Victor Kyomuhendo, Samuel M. Obuchi, Mosol Kandagor Copyright (c) 2025 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1328 Wed, 24 Sep 2025 00:00:00 +0000 Utathmini wa Vitendoneni katika Ngano za Kinyankole https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1358
Makala hii inabainisha vitendoneni katika ngano za Kinyankole na athari za vitendoneni hivyo kwa wasikilizaji. Wanyankole wa jadi walizoea kusimuliana ngano na usimulizi wao ulitumia vitendoneni ambavyo viliathiri hadhira na kuichochea kutenda. Hata hivyo, vitendoneni hivi vilikuwa havijabainika. Makala hii, kwa hiyo, inabainisha, inachanganua na inawasilisha vitendoneni vinavyojitokeza katika ngano za Kinyankole na jinsi vinaathiri hadhira. Uchambuzi wa vitendoneni hivi umeongozwa na nadharia ya Kitendoneni ya Austin (1962). Data ya utafiti imekusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na uchunguzi shirikishi na imetoka kwa watafitiwa 36 ambao tumewateua kimaksudi. Kutoka kwa ngano ishirini tulizokusanya nyanjani, tumechambua ngano saba ambazo tumeteua kinasibu. Uchanganuzi wa data umejikita kwa mkabala wa kiethnografia wa muundo wa kithamano ambao unawasilisha data kiufafanuzi na kimaelezo. Utafiti umegundua kuwa usimulizi wa ngano za Kinyankole unatumia mitindo kisanaa na mitindo hiyo inatumia vitendoneni vinavyoathiri wasikilizaji na kuwachochea kuitikia kwa kutekeleza majukumu mbalimbali. Vitendoneni ambavyo vimebainika ni vya maamuzi, vya maagizo, maagano, maelezo, hisia na vya hulka. Vitendoneni hivi vinaathiri wasikilizaji kwa njia chanya na kwa njia hasi. Kichanya, vinachochea hadhira kutekeleza majukumu kama vile kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza maadili ya kitamaduni. Kihasi, vinaibua mihemuko, huzuni, chuki na hamu ya kulipiza kisasi. Makala hii imehitimisha kwamba vitendoneni vinavyotumiwa katika usimulizi wa ngano za Kinyankole vinachangia uimarishaji wa maadili na utekelezaji majukumu fulani.
Benon Mukundane, Magdaline Wafula, Nathan Ogechi Copyright (c) 2025 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 https://utafitionline.com/index.php/jkal/article/view/1358 Wed, 15 Oct 2025 00:00:00 +0000