Athari ya Upokezi wa Matendo ya Utu kwa Binadamu: Mfano wa Riwaya za Said Ahmed Mohamed
Keywords:
Athari, Binadamu, Utu, Viumbe wa kiuhalisiajabuAbstract
Ili pawepo na mahusiano mema kati ya binadamu, lazima pawepo na utu. Utu, hasa huhusishwa na binadamu. Hali kadhalika, huhusisha wema wowote unaomtendea mtu. Waandishi mbalimbali wa fasihi ya Kiswahili wamedhihirisha utu katika utunzi wao. Mtu anapopokea tendo la utu, huathirika kwa namna mbalimbali. Makala haya yanachunguza athari ya upokezi wa matendo ya utu kwa binadamu. Lengo kuu la makala ni kueleza binadamu anavyoathirika kwa njia mbalimbali kutokana na utu wa viumbe wa kiuhalisiajabu. Viumbe wa kiuhalisiajabu kama wanavyoitwa ni viumbe wenye sifa za kiajabuajabu. Ni viumbe tofauti na binadamu halisi na wenye nguvu fulani. Kutokana na nguvu hizo, huweza kufanya matendo mbalimbali. Makala iliongozwa na nadharia ya kiuhalisiajabu kama inavyofafanuliwa na Zamora na Wendy (1995). Muundo wa kimaelezo ulitumika huku eneo la utafiti likiwa fasihi ya Kiswahili, utanzu wa Riwaya. Sampuli ya kimakusudi ilitumika kuteua riwaya tatu za Said A. Mohamed hususan: Babu Alipofufuka (2001), Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Data ilikusanywa kutokana na kusoma riwaya hizo tatu zilizoteuliwa na kudondoa sehemu zilizolingana na malengo ya utafiti. Data ilidondolewa, ikanukuliwa, ikapangwa kisha kuchanganuliwa. Matokeo yalionyesha kuwa viumbe wa kiuhalisiajabu walidhihirisha utu kwa binadamu kwa namna mbalimbali na athari yake ikabainika. Utafiti huu unatoa mchango kwa walimu na wataalamu wa fasihi katika taaluma ya fasihi simulizi.
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.