Matumizi ya Lugha katika Mandhari-Lugha ya Mji wa Njombe: Uchanganuzi wa Maandishi Katika Mabango ya Pikipiki
DOI:
https://doi.org/10.58721/jkal.v3i1.993Keywords:
Dhima, Maana, Mandhari-lugha, Semiotiki ya kijamiiAbstract
Makala haya yamechunguza matumizi ya lugha katika mandhari-lugha ya mji wa Njombe, kwa kujikita katika maandishi yanayopatikana kwenye mabango ya pikipiki mjini humo. Lengo la utafiti lilikuwa ni kubainisha lugha inayotumika katika mabango ya pikipiki mjini Njombe. Aidha, utafiti ulilenga kuchanganua matumizi ya lugha katika muktadha wa jamii husika. Makala yaliongozwa na Nadharia ya Semiotiki ya Kijamii kama ilivyofafanuliwa na Michael Halliday (1978). Nadharia hii husisistiza kwamba lugha inaweza kuchunguzwa kikamilifu katika vipengele vya maana na dhima kwa kuihusisha na muktadha wa matumizi katika jamii husika. Data zilikusanywa kwa njia ya ushuhudiaji, upigaji picha na mahojiano huru. Data zilizokusanywa ziliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo na takwimu. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa 83.5% ya maandishi kwenye mabango ya pikipiki yalitumia lugha ya Kiswahili. Asilimia 16.5 ya maandishi iliyobaki ilijikita katika vikundi vitatu vya matumizi ya lugha, kila kikundi kikichukua 5.5%. Vikundi hivyo ni pamoja na maandishi yaliyochanganya Kiswahili na lugha ya kiasili, yale yaliyokuwa ya lugha ya kiasili pekee na yale ya lugha ya kigeni pekee. Aidha, ilibainika kuwa maandishi kwenye mabango ya pikipiki yalitumika kutekeza dhima mbalimbali kama vile kuhimiza umuhimu wa bidii na kazi, uadilifu, na uvumilivu. Isitoshe, baadhi ya maandishi yalitumika kujitambulisha na kujinasibisha, kuonyesha imani ya dini katika maisha ya binadamu pamoja na kubainisha uhuru alionao mtu katika kufanya maamuzi. Uelewa wa dhima hizi ulitokana na uelewa wa maana ya maandishi kwenye mabango hayo uliojikita katika muktadha wa jamii husika.
Downloads
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
License

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
