Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1452

Authors

Keywords:

Fasihi, Kiswahili, Sanaa, Tamthiliya

Abstract

Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na thieta ya umma ama sanaa kwa maendeleo ya jamii. Vitabu vyake vya tamthiliya vimeonesha namna alivyochangia katika maendeleo ya tamthiliya kwa kuanzisha mbinu ya usimulizi wa kingano katika tamthiliya zake pamoja na thieta ya umma ili kusadifu utamaduni wa Kibantu. Pia, amesaidia katika kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuongeza msamiati kupitia utunzi wake.  Licha ya mchango wake huo katika tamthiliya na sanaa za maonyesho, mwandishi huyu hajachunguzwa kinagaubaga ili kubaini mchango wake katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. Watafiti mbalimbali wamechunguza baadhi ya kazi zake na kumtaja kuwa ana mchango mkubwa katika fasihi pasipo kuchambua mchango huo (Mutembei 2008; Msemwa 2012 na Sayi 2023). Kutokana na umuhimu wa mtaalamu huyu katika uwanja wa fasihi, hususani katika uwanja wa tamthiliya, ndipo makala hii inakusudia kuchunguza maisha ya Penina Muhando na mchango wa kazi zake katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. Data zilizomo ndani ya makala hii zimetokana na usomaji makini wa kazi zake pamoja na mahojiano baina ya mtafiti na mtafitiwa nyanjani kuhusu mchango wake katika fasihi ya Kiswahili. Makala hii inaongozwa na Nadharia ya Uhalisia iliyoibuka karne ya 19 ili kupinga Tapo la Uromansia. Nadharia hii inasisitiza usawiri wa matukio au maisha katika fasihi kama yalivyo katika maisha ya kila siku. Kupitia nadharia hii tumebaini kuwa Penina Muhando amechangia kukuza fasihi ya Kiswahili kwa kutumia lugha ya Kiswahili, kuingiza maudhui ya dini za Kiafrika katika fasihi na kuhamasisha masuala ya usawa wa kijinsia. Kadhalika, mwanzilishi wa Thieta ya Umma, fasihi ya majaribio ya Kiafrika pamoja na nadharia za fasihi ya Kiswahili.

Published

2025-11-23

How to Cite

Kyamba, A. N. (2025). Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 99–107. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1452

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 3 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.