Mchomozo wa Kiisimu katika Vichwa vya Habari vya Magazeti ya Kiswahili nchini Tanzania: Uchambuzi wa Kimtindo
DOI:
https://doi.org/10.58721/mqdj7d80Keywords:
Magazeti, Mchomozo wa kiisimu, Sintaksia, UmtindoAbstract
Makala hii inachunguza mchomozo wa kiisimu unaojitokeza katika vichwa vya habari vya magazeti ya Kiswahili nchini Tanzania kwa kuongozwa na Nadharia ya Umtindo. Lengo ni kubainisha mbinu za kimtindo zinazotumiwa katika vichwa vya habari na kufafanua mchango wake katika ujenzi wa maana na mvuto wa ujumbe. Data zilikusanywa kutoka magazeti sita ya Kiswahili nchini Tanzania kwa kutumia usampulishaji lengwa na kuchambuliwa kwa mkabala wa kimaelezo na uchambuzi wa kimaudhui. Matokeo yanaonesha kuwa waandishi hutumia mchomozo wa kiisimu kupitia tamathali za semi, ubunifu wa kimsamiati, mkengeuko wa kisintaksia, pamoja na uradidi wa sauti na mchezo wa lugha. Mbinu hizi hutumiwa si kwa ajili ya kupamba lugha pekee, bali pia kufupisha ujumbe, kusisitiza taarifa, kuibua taswira na hisia, kuchochea udadisi na kuongeza uwezekano wa kichwa cha habari kukumbukwa. Hata hivyo, matumizi ya lugha yenye mvuto mkubwa yanaweza wakati mwingine kusababisha utata wa maana au kuathiri usahihi wa uwasilishaji wa taarifa. Makala inahitimisha kuwa mchomozo wa kiisimu ni mkakati muhimu wa kimawasiliano unaowezesha magazeti ya Kiswahili kuunganisha ufupi wa taarifa na mvuto wa lugha, huku ukihitaji matumizi yanayozingatia uwazi na usahihi wa habari.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Journal of Kiswahili and Other African Languages

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.






