Usawiri wa Mwanamke wa Kimfumojike Katika Tamthilia za Kiswahili: Uchambuzi wa Mama Mtakatifu (1982) na Kivuli Kinaishi (1990)

Authors

  • Felix Kwame Sosoo University of Ghana, Legon

DOI:

https://doi.org/10.58721/3kg86r52

Keywords:

Mama mtakatifu, Mfumojike, Ufeministi wa Kiafrika, Usawiri wa mwanamke

Abstract

Makala hii inachunguza usawiri wa mwanamke wa kimfumojike katika tamthilia za Kiswahili kwa kurejelea Mama Mtakatifu (1982) ya Felix Osodo na Kivuli Kinaishi (1990) ya Said Ahmed Mohamed. Lengo ni kubainisha namna mwanamke anavyosawiriwa katika nafasi za mamlaka, uongozi, na uwajibikaji wa kijamii. Utafiti umetumia mkabala wa kitaamuli, ambapo data zimepatikana kupitia usomaji wa kina wa tamthilia teule na kuchanganuliwa kwa kutumia uchanganuzi wa kimaudhui. Nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika imetumika kuongoza ufafanuzi wa nafasi ya mwanamke kwa kuzingatia mazingira ya Afrika ya kijamii, kiutamaduni, na kihistoria. Matokeo yanaonesha kuwa tamthilia hizi zinamsawiri mwanamke kama kiongozi wa ngazi ya juu, mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi, msimamizi wa shughuli za kiutamaduni na ustawi wa jamii, mshiriki katika uongozi wa baraza la wazee, mrithi wa madaraka, na mhusika mwenye hekima, nguvu za kiroho na uwezo wa uganga. Usawiri huu unaonesha kuwa fasihi ya Kiswahili inaweza kuibua mifumo ya kijamii inayompa mwanamke mamlaka na nafasi kubwa katika uendeshaji wa jamii. Hivyo, makala inachangia mjadala kuhusu uwakilishi wa mwanamke kwa kuonesha taswira inayotofautiana na ile ya mwanamke tegemezi katika mifumo ya kimfumodume, na kusisitiza umuhimu wa kuchunguza mazingira ya kijamii yanayounda mamlaka ya wanawake.

Downloads

Published

2026-10-03

Issue

Section

Articles

How to Cite

Usawiri wa Mwanamke wa Kimfumojike Katika Tamthilia za Kiswahili: Uchambuzi wa Mama Mtakatifu (1982) na Kivuli Kinaishi (1990). (2026). Journal of Kiswahili and Other African Languages, 4(2), 1-12. https://doi.org/10.58721/3kg86r52

Similar Articles

1-10 of 47

You may also start an advanced similarity search for this article.