Uhifadhi wa Utamaduni kupitia Mchakato wa Tafsiri: Mifano ya Tafsiri ya Riwaya za Kaburi Bila Msalaba na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka, Ntulanalwo na Bulhawali
Keywords:
Skopos, Tafsiri, Uhifadhi, UtamaduniAbstract
Tafsiri ni mchakato wa kuhawilisha mawazo au ujumbe ulio katika lugha ya maandishi kutoka lugha chanzi kwenda katika lugha lengwa. Taaluma ya tafsiri inatumika kama nyenzo ya kueneza utamaduni, maarifa mapya, ujuzi, na uzoefu kutoka kwa jamii moja kwenda nyingine. Makala hii inakusudia kueleza jinsi utamaduni wa Kiafrika unadumishwa na kuhifadhiwa kupitia mchakato wa tafsiri. Makala iljikita katika uchanganuzi wa tafsiri ya Kaburi Bila Msalaba (1969) na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali (1981). Makala hii ilipania kutoa maelezo jinsi tafsiri ya riwaya hizi ambazo ni hazina ya hifadhi ya utamaduni wa Kiafrika, inavyochangia na kuendeleza uhifadhi wa utamaduni kutoka lugha moja hadi nyingine. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Skopos inayosisistiza lengo la tafsiri kuzingatiwa kabla ya zoezi la tafsiri kuanza. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kusoma na kuchambua matini chanzi Kaburi Bila Msalaba na Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulhawali na matini lengwa, Unmarked Grave na Mr. Myombekere and His Wife Bugonoka, Their son Ntulanalwo and Daughter Bulihwali. Makala hii ililenga kuangazia vipengele vya kitamaduni vilivyohawilishwa kutoka utamaduni chanzi na kuingizwa kwa utamaduni lengwa na jinsi vinavyochangia uhifadhi wa utamaduni katika jamii mahususi. Mkabala wa kitaamuli ulitumika katika uwasilishaji wa data. Matokeo yalidhihirisha kwamba vipengele vya kitamaduni vimehawilishwa kutoka lugha moja kwenda nyingine hivyo basi, uhifadhi wa utamaduni umewezeshwa kupitia mchakato wa tafsiri.
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.