Uhakiki wa Itikadi Zilizofumbatwa Kijazanda kwenye Nyimbo za Kiasili za Kikamba

https://doi.org/10.58721/jkal.v2i2.687

Authors

Keywords:

Asilia, Itikadi, Jazanda, Nyimbo

Abstract

Makala haya yanachunguza itikadi zilizofumbatwa kijazanda katika nyimbo za kiasili za Kikamba. Lengo kuu la makala ni kuhakiki itikadi za Wakamba zinazofumbatwa kijazanda kwenye nyimbo teule. Uchunguzi huu ni wa kithamano. Mbinu ya kimaelezo ilitumika katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Data ya kimsingi ilitokana na nyimbo nane za kiasili za Kikamba zinazosheheni jazanda. Nyimbo zenyewe zilikusanywa kutoka Tume ya Permanent Presidential Music Commission nchini Kenya. Uteuzi huo ulifanyika kimaksudi kwa maana utafiti ulilenga kuhakiki itikadi zinazofumbatwa kijazanda kwenye nyimbo teule. Data ya uchunguzi huu imechanganuliwa na maelezo kutolewa kulingana na lengo la utafiti na mihimili ya kinadharia. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Jazanda Dhanifu na ile ya Itikadi. Kimsingi, huu ni utafiti wa maktabani kwa kuwa data muhimu zilitokana na rekodi zilizowekwa. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa nyimbo za kiasili za Kikamba huwasilisha itikadi za Wakamba zilizofumbatwa kijazanda. Itikadi zenyewe zimejikita katika masuala kama vile tohara, kazi, ndoa na mapenzi, ubikira, utamaduni, malezi na mauti. Matokeo ya utafiti huu yanakuza maarifa kuhusiana na dhima ya kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi za Kiafrika. Makala haya yanapendekeza kwamba ufasiri wa jazanda kwa mujibu wa nadharia ya Udenguzi ufanywe ili kubaini fasiri mbalimbali kwa mujibu wa hadhira.

Published

2024-08-29

How to Cite

Mue, E. K., Wafula, M. N., & Oduori, R. (2024). Uhakiki wa Itikadi Zilizofumbatwa Kijazanda kwenye Nyimbo za Kiasili za Kikamba. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 2(2), 34–43. https://doi.org/10.58721/jkal.v2i2.687

Issue

Section

Articles