Mikakati ya Utetezi wa Mazingira katika Riwaya za Nakuruto na Bustani Ya Edeni

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1105

Authors

Keywords:

Majukwaa, Mazingira, Uhakiki-Ikolojia, Utetezi

Abstract

Makala haya yanalenga kutathmini utetezi wa mazingira katika riwaya za Nakuruto (2009) ya Clara Momanyi na Bustani ya Edeni (2001) ya Emmanuel Mbogo. Kufuatia uharibifu wa mazingira kote ulimwenguni, utetezi wa mazingira umekuwa ukifanyika katika majukwaa mbalimbali yakiwemo makongamano ya kimataifa, mashirika ya uanaharakati na katika vyombo vya habari. Katika miaka ya hivi karibuni wanafasihi pia wameanza kutumia fasihi kama jukwaa la utetezi wa mazingira katika kazi zao za riwaya, tamthilia, hadithi fupi na ushairi. Jambo hili ndilo lililomvutia mtafiti kuchunguza namna suala la utetezi wa mazingira lilivyoshughulikiwa katika riwaya teule. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki-Ikolojia kwa mujibu Glotfelty (1996). Muundo wa utafiti huu ni wa kimaelezo. Sampuli ya utafiti huu ni riwaya za Nakuruto (2009) na Bustani ya Edeni (2001) ambazo ziliteuliwa kimakusudi ili zichunguzwe. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa mikakati mbalimbali kama vile dini, sheria, vyombo vya habari, mabango, nyimbo na maandamano imetumika kuyatetea mazingira. Makala haya yatawachochea wanaharakati wa mazingira katika kutumia majukwaa mbalimbali kuyatetea mazingira. Aidha, utafiti huu utapiga jeki juhudi za Wizara ya Mazingira katika kuhamasisha jamii kuhusu uharibifu dhidi ya mazingira.

Published

2025-06-24

How to Cite

Maina, E., Akaka, L., & Mavisi, R. (2025). Mikakati ya Utetezi wa Mazingira katika Riwaya za Nakuruto na Bustani Ya Edeni . Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 1–9. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1105

Issue

Section

Articles