Mchango wa Muziki wa Bongo Fleva katika Kuibua Msamiati Mpya na Maana Mpya za Kiswahili nchini Tanzania

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1447

Authors

Keywords:

Bongo Fleva, Ethnopragmatiki, Msamiati, Muziki

Abstract

Makala hii inachunguza jinsi muziki wa Bongo Fleva unavyochangia katika kuibua msamiati mpya na kutoa maana mpya katika lugha ya Kiswahili nchini Tanzania. Kwa kutumia Nadharia ya Uchanganuzi wa Maana katika Muktadha wa Jamii (Ethnopragmatiki), makala inachambua jinsi lugha inavyotumika katika mazingira halisi ya kijamii na kitamaduni. Makala hii ilitumia mbinu ya uchambuzi wa maudhui, ambapo nyimbo kumi (10) za Bongo Fleva zilichaguliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa ili kubaini mabadiliko ya msamiati na maana. Data zilipatikana kutoka kwenye tovuti zinazohifadhi nyimbo “lyrics” kama vile “Genius.com” na “LyricFind”. Matokeo yanaonesha kuwa muziki wa Bongo Fleva unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuibua maneno mapya na kubadilisha maana ya maneno yaliyokuwepo. Hii ni kwa kuwa Wasanii wanatumia lugha ya taswira, mafumbo, na msamiati wa kisasa kuakisi masuala ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi. Pia, uchunguzi unaonesha kuwa Bongo Fleva si tu burudani, bali chombo cha kuboresha na kuendeleza Kiswahili, huku ukichangia katika ukuaji wa msamiati na uhamasishaji wa matumizi ya lugha katika jamii.  Hivyo, wataalamu wa lugha na jamii hawana budi kutambua na kuthamini mchango huu muhimu katika ukuaji wa Kiswahili kama lugha hai na inayobadilika.

Published

2025-11-23

How to Cite

Haonga, E. D. (2025). Mchango wa Muziki wa Bongo Fleva katika Kuibua Msamiati Mpya na Maana Mpya za Kiswahili nchini Tanzania . Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 89–98. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1447

Issue

Section

Articles

Similar Articles

You may also start an advanced similarity search for this article.