Sababu za Kupungua kwa Matumizi ya Majina ya Asili Nchini Tanzania: Mifano Kutoka Ginantuzu Lahaja ya Kisukuma
Keywords:
Athari, Ginantuzu, Kupungua, Majina ya AsiliAbstract
Miaka ya hivi karibuni majina ya asili yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya kupotea kwa kasi isiyo kifani hasa kwa vijana nchini Tanzania. Makala hii imechunguza sababu za kupungua kwa matumizi ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu, mojawapo ya lahaja za Kisukuma. Makala imeongozwa na baadhi ya maswali. Maswali hayo ni: Kwa nini majina ya asili yanapungua kila kukicha nchini Tanzania? Nini sababu za kupungua kwa matumizi ya majina ya asili hasa kwa vijana? Nini athari kwa jamii iwapo majina ya asili yakipotea? Data za makala hii zilikusanywa kwa mbinu ya ushuhudiaji, mahojiano, hojaji na mapitio ya nyaraka za maktabani, makavazi na mitandaoni. Makala ilitumia mkabala wa kitaamuli. Matokeo ya makala yameonesha kuwa, sababu za kupungua kwa matumizi ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu ni mwingiliano wa ndoa katika familia, kuingia kwa dini ya Ukristo, kuporomoka kwa maadili kwa vijana, uhamiaji, kukosa umaarufu kwa majina ya asili, kasumba za ustaarabu kwa vijana, baadhi ya majina kupitwa na wakati, kukosa elimu kuhusu majina ya asili, na utandawazi. Aidha, makala pia inaonesha kuwa athari za kupotea kwa majina ya asili ni: kupoteza utambulisho wa jamii, kupoteza utamaduni, na kuhafifisha falsafa asilia za Ginantuzu zilizofumbatwa katika majina hayo. Makala inapendekeza kuwa wanajamii wanapaswa kupewe elimu kuhusu maana ya majina ya asili, pamoja na umuhimu wa kuyatumia. Hii itakuwa njia mwafaka ya kuhifadhi utamaduni, falsafa na historia ya jamii ya Ginantuzi kupitia majina ya asili.
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.