Mofosemantiki na dhima ya Majina ya Ng’ombe kwa Kigezo cha Rangi: Mifano kutoka Jamiilugha ya Ginantuzu

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1155

Authors

Keywords:

Dhima, Majina, Mofosemantiki, Ng’ombe

Abstract

Makala hii inahusu uchunguzi wa mofolojia na semantiki katika majina ya ng’ombe kwa kigezo cha rangi hususani katika jamiilugha ya Ginantuzu. Lengo kuu la makala hii ni kubainisha maumbo yaliyomo katika majina ya ng’ombe, maana na dhima za majina ya ng’ombe. Utafiti huu ulifanywa katika mkoa wa Simiyu, wilaya ya Bariadi vijijini. Jumla ya vijiji viwili vilipitiwa na mtafiti. Vijiji hivyo ni Ihusi na Nkindwabiye. Sampuli ya watoataarifa sita (6) iliteuliwa na mtafiti kwa ajili ya mahojiano ili kukidhi lengo la makala hii. Kwa kutumia usampulishaji lengwa wastani wa watoataarifa (3) kwa kila kijiji walipatikana. Watoataarifa waliteuliwa kwa kuzigatia kigezo cha usampulishaji lengwa. Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano, ushuhudiaji na mapitio ya nyaraka za maktabani na mitandaoni. Ili kufanikisha kazi hii, makala ilitumia nadharia ya Semeotiki iliyoasisiwa na Ferdinand de Saussure. Aidha, Mkabala wa kitaamuli ndio umetumiwa kubainisha maumbo, maana na dhima za majina ya ng’ombe. Matokeo yameonesha kuwa majina ya ng’ombe dume yameundwa kwa mashina ya ng’ombe jike kwa kuongezewa mofu tangulizi inayobeba maana ya dume. Jumla ya alomofu tatu zinazobanisha jinsia ya kiume zilipatikana. Alomofu hizo ni gί-, gid- na gida-. Mwisho makala hii inapendekeza uchunguzi zaidi wa kiisimu kuhusu utoaji wa majina ya mifugo kuendelea kufanyika ili kuimarisha mawasiliano katika jamii mbalimbali za wafugaji na kuyahifadhi majina hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Published

2025-07-16

How to Cite

Masanja, N. (2025). Mofosemantiki na dhima ya Majina ya Ng’ombe kwa Kigezo cha Rangi: Mifano kutoka Jamiilugha ya Ginantuzu. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 30–44. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1155

Issue

Section

Articles