Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Keywords:
Athari, Maarifa, Mtaala, UmilisiAbstract
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwango cha umahiri wa kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari kilikuwa cha chini sana licha ya kufundishwa lugha hiyo kwa kutumia Mtaala wa Maarifa. Utafiti wa awali uliofanywa na watafiti ulibainisha kuwa, kiwango cha umahiri cha wanafunzi kuzungumza lugha ya Kiswahili kimeongezeka tangu kuanza kutumiwa kwa Mtaala wa Umilisi katika ufundishaji mwaka 2020 tofauti na ilivyokuwa chini ya Mtaala wa Maarifa. Kutokana na matokeo hayo, utafiti uliozaa makala haya umetathmini athari za Mtaala wa Umilisi katika ukuzaji wa umahiri wa kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda. Sampuli ya watoataarifa kumi na wawili (12) walimu na ishirini na wanne (24) wanafunzi ilitumika kwenye utafiti huu. Nadharia ya Mawasiliano katika Ufundishaji wa Lugha imetumika katika uchanganuzi wa data za utafiti. Mbinu zilizotumika kukusanya data za utafiti huu ni ushuhudiaji na usaili. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba, athari za Mtaala wa Umilisi katika ukuzaji wa umahiri wa kuzungumza Kiswahili imebainika kuwa mtaala una athari chanya. Athari hizo zipo katika mbinu za ufundishaji, mbinu za ujifunzaji, mawanda ya matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi husika na mawanda ya ujifunzaji na tathmini.
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.


