Kupotea kwa Maneno Chanzi katika Lahaja za Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Lahaja ya Kipemba
Keywords:
Bayana, Chanzi, Kategoria, UsanifishajiAbstract
Tafiti mbalimbali zinaonesha kwamba, baadhi ya lahaja za Kiswahili zinaelekea kupoteza uasili wake kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kijamii na kihistoria. Kupotea kwa maneno chanzi katika lahaja ni tatizo linalohitaji umakini wa haraka kwa sababu huenda kizazi kijacho kisiweze kuyatambua kabisa maneno hayo. Pamoja na ukweli huo, hakujawa na uchunguzi wa kina unaoonesha mifano kuntu ya maneno chanzi ambayo yanaonekana kupotea katika lahaja mbalimbali za Kiswahili ikiwamo lahaja ya Kipemba. Hivyo, makala hii inachunguza mifano ya maneno chanzi yanayoanza kupotea katika lahaja hiyo. Kwa hakika uchunguzi huu utasaidia kuyaweka bayana maneno hayo ili yabaki hai na yaendelee kutumiwa na watafiti pamoja na waandishi mbalimbali wa lugha ya Kiswahili na lahaja zake. Aidha, makala imechunguza sababu pamoja na athari za kupotea kwa maneno chanzi. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa na De Saussure mwanzoni mwa karne ya 20. Data za makala hii zimekusanywa kupitia mbinu ya usomaji wa nyaraka, ushuhudiaji, usaili na hojaji. Makala imebaini kuwa kuna maneno chanzi mbalimbali ambayo yamepotea na mengine yanaendelea kupotea katika lahaja hiyo. Aidha, makala inatoa mchango mkubwa kwa taasisi za BAKITA na BAKIZA kwa kuwa zitaweza kuyatumia maneno hayo katika uundaji na usanifishaji wa istilahi za Kiswahili. Pia, watafiti na waandishi mbalimbali wa lahaja za Kiswahili wataweza kuyatumia maneno hayo katika tafiti zao. Makala imetoa mapendekezo ya kufanyika kwa uchunguzi zaidi wa maneno hayo katika lahaja nyingine mbalimbali za Kiswahili.
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.