Usawiri wa Ujumi katika Fasihi Simulizi: Uchambuzi wa Ngano za Wahehe

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1130

Authors

Keywords:

Sanaa, Fasihi, Fasihi Simulizi , Ngano , Ujumi

Abstract

Lengo la makala hii ni kujadili namna ujumi unavyosawiriwa katika fasihi simulizi, hususani ngano za Wahehe. Kusawiriwa kwa ujumi katika ngano za Wahehe kupitia vipengele vya ujumi kumeweka bayana uwiano wa vipengele hivyo na jamii husika. Aidha, athari zake kwa jamii husika zimebainishwa. Utafiti uliozaa makala hii ulitumia mbinu za kitaamuli. Data zilikusanywa kwa kutumia njia za uchambuzi matini na mahojiano. Ngano teule zilipatikana kwa kutumia sampuli lengwa. Utafiti na mjadala vimefanywa kwa kutumia Nadharia ya Ki-Marx iliyoasisiwa na Karl Marx na Fredrick Engels. Nadharia hii imekuwa faafu katika utafiti wa makala hii kwasababu inatumia mbinu za kipembuzi katika kuchanganua masuala ya kijamii na kiutamaduni. Matokeo yameonesha kwamba ujumi unaweza kusawirika katika ngano za Wahehe kupitia vipengele vyake, ambavyo ni ujumi katika mtu, asili, vitu, na sanaa. Aidha, vipengele hivyo vinaweka wazi idili za jamii husika zinazotokana na masuala mbalimbali yaliyopo kwenye jamii kama vile uongozi, malezi, ndoa, ufugaji, ulinzi, na kilimo.

Published

2025-07-12

How to Cite

Luhwago, N. J. (2025). Usawiri wa Ujumi katika Fasihi Simulizi: Uchambuzi wa Ngano za Wahehe . Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 10–18. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1130

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.