Thamani ya Ukizinda wa Waswahili katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya Teule

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1475

Authors

Keywords:

Riwaya, Thamani, Ukizinda, Waswahili

Abstract

Makala hii inajadili kuhusu usawiri wa thamani ya ukizinda wa Waswahili katika riwaya ya Kiswahili kwa kuzingatia mifano kutoka riwaya teule. Dhana ya ukizinda huweza kutazamwa katika mielekeo mikuu mitatu. Mielekeo hiyo kwa mujibu wa Sanga (2018) na Jumanne (2025) ni mtu, vitu vya asili na sanaa. Ukizinda kama sehemu ya utamaduni wa jamii ya Waswahili, umetafitiwa zaidi katika uga wa Sosholojia (Mhlongo, 2009) kuliko katika uga wa fasihi (Jumanne, 2025). Kwa jamii ya Waswahili, ukizinda  unajitokeza kama kitu chenye thamani kubwa katika utamaduni wao (Sengo, 1992). Data zinazojenga makala hii zimetokana na njia ya uchambuzi wa matini ambapo riwaya za Rosa Mistika (1971) na Harusi (1984) zilisomwa na kuchambuliwa. Aidha, makala hii imetumia mbinu ya usimbishaji wa kimaudhui katika uwasilishaji wa matokeo huku ukiongozwa  na Nadharia ya Uhalisia. Matokeo ya mjadala wa makala hii yanaonesha kuwa ukizinda katika jamii za Waswahili una thamani ya namna tatu. Nazo ni: thamani ya kiutamaduni, kiteolojia na kiujumi.

Published

2025-12-09

How to Cite

Jumanne, A. (2025). Thamani ya Ukizinda wa Waswahili katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya Teule. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 108–117. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1475

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.