Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1479

Authors

Keywords:

Mtagusano, Riwaya, Ubuntu, Utandawazi

Abstract

Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazosawiri mfumo wa maisha unaowaunganisha Waafrika kuishi kwa umoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo (Mbaabu, 1985). Riwaya za mwanzo zilihusisha mambo mbalimbali kama vile kusifia uhuru, falsafa ya Ubuntu, na Azimio la Arusha. Kwa kuwa, falsafa ya Ubuntu ilikuwepo toka zamani, ilichunguzwa pia katika riwaya za mwanzo (Roman, 2019). Vilevile, kuna tafiti zimeonesha kuwa falsafa ya Ubuntu imepotea kipindi cha utandawazi (Masimo, 2023). Hivyo, shabaha ya makala hii ni kuonesha mtagusano wa vipengele vya utandawazi na vya falsafa ya Ubuntu katika riwaya za kisasa za Kiswahili. Inasemekana kuwa, uandishi wa riwaya za kisasa ulianza miaka 1990 hadi sasa, ingawa utafiti huu umehusisha riwaya za kisasa zilizoandikwa miaka 2000 hadi 2010. Hii ni kwa sababu, riwaya zilizoandikwa miaka hiyo ni za aina tofauti, kama vile riwaya za kihistoria, za kisasa, na za kisaikolojia (Mulokozi, 2017). Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva mwaka 1960. Data zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini zinazohusiana na utafiti ambazo ni riwaya za kisasa mbili za Kiswahili, nazo ni Babu Alipofufuka (2001) na Makuadi wa Soko Huria (2002). Riwaya hizo zimeteuliwa kwa sababu, zina sifa inayoendana na mada ya utafiti, na ni miongoni mwa riwaya za kisasa zilizoandikwa miaka 2000 mpaka 2010. Vilevile, data zilizopatikana zilifafanuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli. Aidha, matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa vipengele vya utandawazi vimetagusana na vipengele vya falsafa ya Ubuntu katika riwaya za kisasa.

Published

2025-12-10

How to Cite

Malindi, B., & Kyamba, A. (2025). Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 118–127. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1479

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.