Mitazamo ya Ontolojia ya Waswahili katika Riwaya Teule za Muhammed Said Abdulla

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1500

Authors

Keywords:

Mitazamo, Ontolojia, Riwaya, Waswahili

Abstract

Makala hii inafafanua namna mitazamo ya jamii ya Waswahili katika riwaya teule za Muhammed Said Abdulla (kuanzia sasa ataitwa MSA) inavyostawisha ontolojia yao. Kuwapo kwa suala la mitazamo tofauti katika jamii ya Waswahili limekuwa likishughulisha watafiti wengi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kila jamii ina namna yake ya kuangalia mambo kulingana na vyanzo vyao vya epistemolojia ambavyo kwavyo ontolojia huzaliwa (Sanga, 2018; Khamis, 2022). Hata hivyo, suala hili limekuwa likijadiliwa katika ujumuishi wa Uafrika bila ya kuangalia jamii pwekepweke. Makala hii inabainisha namna riwaya za MSA zinavyodhirisha kuwa mitazamo ya Waswahili ndiyo inayostawisha ontolojia yao. Makala hii imetokana na usanifu wa uchunguzi kifani ambapo data zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi matini. Kupitia mbinu hiyo, jumla ya riwaya tatu (3) zimesomwa na kuchambuliwa. Riwaya hizo ni: Kisima cha Giningi (2011), Duniani Kuna Watu (2017) na Kosa la Bwana Msa (2013). Nadharia ya Ndani-Nje imetumika kwa kukamilishana na mbinu ya usimbishaji wa kimaudhui. Matokeo yanadhihirisha kwamba kuna mitazamo mitatu ya ontolojia ya Waswahili. Mitazamo hiyo ya kiontolojia ni: mtazamo wa imani za kijadi, mtazamo wa imani za kidini na mtazamo wa imani changamani.

Published

2025-12-23

How to Cite

Khamis, T. Y. (2025). Mitazamo ya Ontolojia ya Waswahili katika Riwaya Teule za Muhammed Said Abdulla. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 128–137. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1500

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.