Tamathali za Usemi na Uchimuzi wa Maudhui ya Mamlaka katika Asali Chungu

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1328

Authors

Keywords:

Mamlaka, Mtindo, Uchimuzi, Ukiushi

Abstract

Lengo la makala haya ni kuchunguza jinsi Said Ahmed Mohamed anavyotumia tamathali za usemi mbalimbali kama vipengele vya kimtindo katika kuibua maudhui ya mamlaka katika riwaya yake ya Asali Chungu. Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Uchimuzi, hasa mhimili wa ukiushi wa nadharia hiyo. Data ilikusanywa kwa kunakili madondoo kutoka katika riwaya ya Asali Chungu. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kulenga madondoo yanayochimuza maudhui ya mamlaka katika riwaya hiyo. Uchanganuzi wa data ulifanywa kitaamuli kwa kutambulisha ruwaza na mienendo ya kiisimu iliyobainika katika madondoo. Kisha, uamilifu wa ruwaza na mienendo hiyo ulichanganuliwa kwa kuzingatia muktadha wa ruwaza na mienendo hiyo, mintarafu suala la mamlaka. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba sitiari na kinaya ndizo tamathali za usemi zilizotumiwa hasa na mwandishi kusawiri maudhui ya mamlaka katika riwaya yake. Utafiti huu unapendekeza kwamba uchunguzi kuhusu tamathali za usemi uhusishwe na vipengele vingine vya kimtindo kama vile kipengele cha kileksika na cha kisintaksia. 

Published

2025-09-24

How to Cite

Kyomuhendo, V., Obuchi, S. M., & Kandagor, M. (2025). Tamathali za Usemi na Uchimuzi wa Maudhui ya Mamlaka katika Asali Chungu. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 45–54. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1328

Issue

Section

Articles