Utathmini wa Vitendoneni katika Ngano za Kinyankole

https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1358

Authors

Keywords:

Kuitikia, Kujamiisha, Usimulizi-tendi, Vitendoneni

Abstract

Makala hii inabainisha vitendoneni katika ngano za Kinyankole na athari za vitendoneni hivyo kwa wasikilizaji. Wanyankole wa jadi walizoea kusimuliana ngano na usimulizi wao ulitumia vitendoneni ambavyo viliathiri hadhira na kuichochea kutenda. Hata hivyo, vitendoneni hivi vilikuwa havijabainika. Makala hii, kwa hiyo, inabainisha, inachanganua na inawasilisha vitendoneni vinavyojitokeza katika ngano za Kinyankole na jinsi vinaathiri hadhira. Uchambuzi wa vitendoneni hivi umeongozwa na nadharia ya Kitendoneni ya Austin (1962). Data ya utafiti imekusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na uchunguzi shirikishi na imetoka kwa watafitiwa 36 ambao tumewateua kimaksudi. Kutoka kwa ngano ishirini tulizokusanya nyanjani, tumechambua ngano saba ambazo tumeteua kinasibu. Uchanganuzi wa data umejikita kwa mkabala wa kiethnografia wa muundo wa kithamano ambao unawasilisha data kiufafanuzi na kimaelezo. Utafiti umegundua kuwa usimulizi wa ngano za Kinyankole unatumia mitindo kisanaa na mitindo hiyo inatumia vitendoneni vinavyoathiri wasikilizaji na kuwachochea kuitikia kwa kutekeleza majukumu mbalimbali. Vitendoneni ambavyo vimebainika ni vya maamuzi, vya maagizo, maagano, maelezo, hisia na vya hulka. Vitendoneni hivi vinaathiri wasikilizaji kwa njia chanya na kwa njia hasi. Kichanya, vinachochea hadhira kutekeleza majukumu kama vile kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza maadili ya kitamaduni. Kihasi, vinaibua mihemuko, huzuni, chuki na hamu ya kulipiza kisasi. Makala hii imehitimisha kwamba vitendoneni vinavyotumiwa katika usimulizi wa ngano za Kinyankole vinachangia uimarishaji wa maadili na utekelezaji majukumu fulani.

Published

2025-10-15

How to Cite

Mukundane, B., Wafula, M., & Ogechi, N. (2025). Utathmini wa Vitendoneni katika Ngano za Kinyankole. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 3(2), 55–65. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1358

Issue

Section

Articles