Uchunguzi wa Usawiri wa Nadharia ya Udhanaishi katika Misemo ya Kiswahili
(Translation: An Examination of the Portrayal of Existentialism Theory in Swahili Sayings)
Keywords:
Kifo, Maisha, Misemo, Nadharia, UdhanaishiAbstract
Makala hii inachunguza usawiri wa Nadharia ya Udhanaishi katika misemo ya Kiswahili. Nadharia ya Udhanaishi inahoji kuhusu kifo na maana ya maisha. Kila jamii inafungamana na imani, itikadi, mwelekeo na falsafa mahususi. Uhai, maisha na kifo hufasiliwa na jamii kupitia lugha na fasihi ya jamii husika. Swali ambalo tunajiuliza ni je, misemo ya Kiswahili inayotumiwa katika maisha ya kila siku imefungamana na kusawiri Nadharia ya Udhanaishi? Hivyo, makala hii imelenga kuchunguza usawiri wa Nadharia ya Udhanaishi katika misemo ya Kiswahili. Lengo la makala hii ni kubainisha usawiri wa udhanaishi katika misemo ya Kiswahili na maana zake. Data zilikusanywa kwa njia ya usomaji makini na dodoso. Aidha, makala hii imetumia mihimili ya Nadharia ya Udhanaishi katika kuchunguza, kuchambua na kujadili usawiri wa udhanaishi katika misemo ya Kiswahili. Makala hii inajadili kwamba, Nadharia ya Udhanaishi inafungamana na maisha ya kila siku ya jamii ya Kiswahili na inasawiriwa katika misemo inayotumiwa kila siku. Hivyo, watu ni waumini wa udhanaishi bila kujua ama kujitanabiasha kama wadhanaishi kupitia misemo wanayotumia katika kuyasawiri maisha na mazingira yao ya kila siku.
Translation (English)
Abstract
This article explores the representation of existentialist theory within Swahili sayings. Existentialist theory interrogates the concepts of death and the meaning of life. Distinct beliefs, ideologies, orientations, and philosophies unite each society. Societies interpret life, living, and death through their unique languages and literatures. We ponder whether Swahili sayings employed in daily life inherently reflect existentialist theory. Thus, this article investigates the representation of existentialism in Swahili sayings to understand how existentialism is conveyed. This paper seeks to identify the portrayal of existentialist theory in Swahili sayings and their meanings. The data for this study were gathered through critical reading and questionnaire methods. The paper employs the principles of existentialist theory to examine, analyse, and discuss the depiction of existentialism in Swahili sayings. It posits that existentialist theory is intricately linked to the daily lives of Swahili society and is reflected in the sayings used in everyday contexts. As a result, individuals may believe in existentialism without consciously recognising it or labeling themselves as existentialists, as reflected through the sayings they utilize to depict their daily lives and environments.
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.