Umuhimu wa Uundaji wa Wahusika Mviringo katika Riwaya za Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Rosa Mistika

Authors

  • Gervas A. Kasiga University of Dodoma, Tanzania

DOI:

https://doi.org/10.58721/xapqnt19

Keywords:

Fasihi, Kiswahili, Sanaa, Wahusika mviringo

Abstract

Makala hii inajadili umuhimu wa uundaji wa wahusika mviringo katika riwaya za Kiswahili. Riwaya ya Rosa Mistika (1971) ya Euphrase Kezilahabi imetumika kuonesha namna wahusika mviringo wanavyowasilisha ujumbe kulingana na uhalisia wa mabadiliko ya mwanadamu. Mbinu za uchambuzi matini na mahojiano zilitumika katika ukusanyaji wa data. Nadharia ya Uhalisia imetumika katika mchakato mzima wa ukusanyaji data, uchambuzi data, na matokeo yake. Matokeo yamebainisha kuwa uundwaji wa wahusika mviringo katika riwaya za Kiswahili una umuhimu katika kuonesha mabadiliko ya mwanadamu, kuimarisha uhalisia wa matukio ya riwaya, pamoja na kusaidia kuibua migogoro ya ndani na nje ya wahusika. Zaidi, ilibainika kuwa uviringo husaidia kuendeleza maudhui na kuongeza mvuto wa kisanaa wa riwaya. Kwa kuzingatia mjadala uliofanyika, makala imehitimisha kwa kauli kuwa, wahusika mviringo ni nyenzo muhimu ya kisanaa inayosaidia riwaya za Kiswahili kuwasilisha maisha ya binadamu kwa uhalisia pamoja na kuifanya kazi ya fasihi kuwa na mvuto wa kisaikolojia na kijamii.

Downloads

Published

2026-10-17

Issue

Section

Articles

How to Cite

Umuhimu wa Uundaji wa Wahusika Mviringo katika Riwaya za Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Rosa Mistika. (2026). Journal of Kiswahili and Other African Languages, 4(2), 27-39. https://doi.org/10.58721/xapqnt19

Similar Articles

1-10 of 35

You may also start an advanced similarity search for this article.