MABADILIKO YA KIMAANA KATIKA METHALI ZA KIJINSIA: MIFANO KUTOKA JAMII YA WANYANKOLE

Authors

  • Arinaitwe Annensia Chuo Kikuu cha Moi
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi
  • Magdaline Wafula Chuo Kikuu cha Moi

DOI:

https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.94

Keywords:

Jinsia, Kinyankole, Maana, Mabadiliko

Abstract

Makala hii inachunguza mabadiliko kimaana na kimatumizi katika methali za kijinsia katika jamii ya Wanyankole. Lengo kuu la makala hii ni kubainisha athari ya mabadiliko katika jamii kwa kujikita kwenye ufasiri wa maana na matumizi ya methali za kijinsia miongoni mwa Wanyankole nchini Uganda. Mbinu za mahojiano zilitumika katika ukusanyaji wa data. Utafiti huu ulihusisha methali kumi na tano za kijinsia katika jamii ya Wanyankole. Uteuzi huo ulifanyika kimaksudi kwa kuwa utafiti ulilenga kuchanganua methali zilizohusu jinsia za kike na kiume katika jamii ya Wanyankole. Nadharia ya Udenguzi ilitumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa kadri ulimwengu unavyobadilika ndivyo jamii ya Wanyankole inavyobadilika. Hivyo basi mabadiliko haya yameathiri ufasiri wa maana na matumizi katika methali za kijinsia za Wanyankole. Makala hii inapendekeza kuwa baadhi ya methali zinafaa kuchunguzwa upya kiufasiri, kimuundo na kimatumizi ili uamilifu wake uwiane na jamii ya kisasa.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2023-05-19

How to Cite

Annensia, A. ., Kandagor , M. ., & Wafula , M. . (2023). MABADILIKO YA KIMAANA KATIKA METHALI ZA KIJINSIA: MIFANO KUTOKA JAMII YA WANYANKOLE. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 1(1), 1–8. https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.94

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.